Benki ya Stanbic Tanzania, ambayo ni kiungo muhimu katika sekta ya huduma za kibenki nchini Tanzania, na Ramani, kampuni namba moja kwenye teknolojia ya kifedha, wanafurahi kutangaza ushirikiano uliolenga kuleta mabadiliko kwenye sekta ya biashara, nakuendeleza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini  kwa ufanisi zaidi. 

Ushirikiano huu wa kipekee unalenga kutumia teknolojia na msaada mkubwa wa kifedha, kuimarisha uwezo wa biashara za wasambazaji wa ndani na wajasiriamali.

Muunganiko huu unalenga kutumia miundombinu yakifedha ya kisasa ya Kampani ya Ramani, pamoja na rasilimali imara za kifedha za Benki ya Stanbic.

Pia, utasaidia zaidi ya wasambazaji 100 katika mwaka wake wa kwanza, ukiangazia mnyororo muhimu wa thamani katika sekta ya Bidhaa za Watumiaji (FMCG). 

Pamoja na majukwaa ya teknolojia ya hali ya juu na mikakati ya kifedha, ushirikiano huu utakabiliana na vipengele muhimu vya usimamizi wa biashara, ufuatiliaji wa mauzo, na miamala ya kidijitali ili kuongeza ufanisi wa uendeshaji kwa wasambazaji.

Fredrick Max, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benkiya Stanbic Tanzania, alisema, "Ushirikiano wetu na Ramani ni zaidi ya biashara; ni ushirikiano wa kimkakati ambao unaahidi kubadilisha jinsi biashara inavyofanywa nchini Tanzania. 

Kwa kuunganisha nguvu zetu na maono yetu, tunapanga kusaidia mahitaji ya kifedha ya wasambazaji wa ndani, na pia kuchangia kwa kiasiki kubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu."

Lengo kuu ni kutoa fedha kwa wasambazaji na wauzaji ili kuboresha usimamizi wa ugavi kwa wasambazaji na wafanyabiashara wa bidhaa kubwa. 

Hii itawezesha usimamizi bora wa manunuzi, udhibiti wahisa na ufuatiliaji wa mauzo ya kidijitali katika kuimarisha michakato ya biashara na miamala yakifedha.

Iain Usiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampani ya Ramani, alisema, "Tunafurahi kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania. Ushirikiano huu utarahisisha na kuimarisha usimamizi wa wasifu wa mikopo na kukuza huduma za kifedha.  Tunable mabadiliko chanya katika kuendesha biashara, na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha."


Mafanikio ya ushirikiano huu yatapimwa nauandikishwaji wa wafanyabiashara 100 katika mwaka wakwanza, na mipango ya kukuza ufikiaji kwa kiasikikubwa, ili kufikia biashara zaidi nchini Tanzania.

Takwimu za mitandao ya kijamii, ukuaji wa kifedha, naviwango vya kuandikisha wateja, zitatumika kamaviashiria muhimu vya mafanikio na ufanisi wamuunganiko huu.

Ushirikiano kati ya Benki ya Stanbic Tanzania na Ramani, unatengeneza kiwango kipya cha ushirikiano katika sekta ya kifedha na teknolojia, huku ukionyeshamatumaini makubwa katika kuboresha jinsi biasharainavyofanywa na kusaidiwa kifedha nchini Tanzania.

Kupitia hatua hii, mashirika yote mawili yanathibitishatena azma yao ya kuchochea ukuaji wa kiuchumi, nakuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwaWatanzania wote.


Na. Josephine Majura, WF, Dodoma

Serikali imesema kuwa inaandaa mfumo wa kielektroniki wa kutoa ankara ya pamoja kwa huduma zinazolandana ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaostahili kulipa kodi ya jengo na kodi ya ardhi.

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,  Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuziunganisha kodi ya jengo na kodi ya ardhi.

“Serikali kupitia Kamati ya Moberesho ya Mfumo wa Kodi inaendelea kufanya uchambuzi na tathmini ya mifumo ya kodi, ada na tozo za huduma kwa lengo la kuondoa urasimu na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini”, alisema Mhe. Chande.

Alisema tathmini hiyo inajumuisha mapendekezo ya maboresho ya mfumo wa usimamizi wa kodi ya jengo na kodi ya ardhi kama inavyopendekezwa na Mheshimiwa Khamis. 

Aidha katika swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Mwera Mhe. Zahor Mohamed Haji, alitaka kujua mpango wa Serikali wa utoaji elimu kwenye mifumo inayoanzishwa. 

Mhe Chande alisema kuwa Serikali kupitia Taasisi zake imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu siku hadi siku kwa wadau wake kulingana na uhitaji katika kipindi hicho.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuziunganisha kodi ya jengo na kodi ya ardhi.



SERIKALI kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kuwa ina lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tarafa hiyo kwa kuwaelimisha na kuwahamisha wananchi waliojiandikisha kuhama kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga na maeneo mengine nchini.

Akizungumza na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwa nyakati tofauti katika zoezi la uelimishaji, uhamaishaji na uandikishaji kaimu meneja wa Uhusiano kwa Umma wa mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema zoezi la kuwaelimisha wananchi hao litaendelea ili kuhakikisha kila mkazi wa tarafa ya Ngorongoro anahama kwa hiyari.

Amewaeleza wananchi hao kwamba serikali haina nia mbaya kwa kuwashawishi kuhama kutoka ndani ya hifadhi kwani inatambua kuwa iwapo wananchi hao watakubali kuhama wataweza kuboresha maisha yao katika maeneo mbalimbali watakayoamua kuelekea sambamba na kulinda usalama wao kutokana na uwepo wa matukio ya wanyama wakali ndani ya hifadhi.

“Mnaishi katika mazingira magumu hasa kutokana na kukosa uhuru wa kuingia na kutoka ndani ya hifadhi, kuhofia Wanyama wakali ambao wamekuwa hatari kwa mifugo na baadhi ya wananchi, serikali imefanya uamuzi sahihi wa kuwahamasisha ili kuwa na Maisha bora na huru nje ya hifadhi,”alisema bwana Dambaya.

Bwana Dambaya amesisitiza kuwa serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mwananchi anayekubali kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi anapata stahiki zake zote za kisheria ikiwemo kitita cha shilingi milioni kumi wanaohamia msomera na shilingi Milioni kumi na tano wanaohamia maeneo mengine ambapo fedha hizi zinatolewa kama motisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Amewataka wananchi hao kuachana na propaganda za baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wasiowatakia mema kwa kuwashawishi kuendelea kubaki ndani ya hifadhi huku wao na familia zao wakiishi katika miji mbalimbali nchini na kufanya shughuli zao katika mazingira magumu.

“Msihadaike na watu wenye nia ovu wanaowashawishi mbaki ndani ya hifadhi, hameni kwa hiyari kuelekea katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine ambayo huduma za kijamii zimeboreshwa kwa mustakabali wenu na vizazi vyenu”,alisema bwana Dambaya.

Katika ziara hiyo ya tarafa ya Ngorongoro timu ya uhamasishaji imeweza kutembelea kaya mbalimbali katika Kijiji cha Naiyobi, Kapenjiro na endulen ambapo wananchi kadhaa walielimishwa na kukubali kuhama kwa hiyari na kuamua kujiandikisha.
Na Nihifadhi Issa Zanzibar.
SHERIA ya Ofisi ya Mufti wa Zanzibar ya mwaka 2021 kwenye kipengele cha ufafanuzi imefafanua Ulamaa kuwa ni “ Mwanachuoni wa Kiislamu mwenye elimu ya kutosha ya fani mbalimbali ya dini ya kiislam na lugha ya kiarab”. Hapana hakuna sehemu iiyowekwa jinsia maana wanawake na wanaume wenye uwezo wa kielimu wapewe nafasi. Ila suala hili kwa baadhi ya dini ni jambo lisilopewa kipaombele.

Sheikh Khamis Shabaan Khamis ni Iman wa Msikiti pia ni Kiongozi wa dini anayepinga suala la wanaume kuona na kuzungumza kuwa wanawake hawana haki ya kuwa kwenye sehemu za maamuzi, amesema suala la kuharamisha na kuhalilisha suala lolote la kidini ni jambo ambalo linatakiwa litokane na Quran na Mafundisho ya Mtume Muhammad (S.W.A).”Kumzuia mwanamke asishiriki katika utowaji wa Fatwa au maamuzi, kumharimisha wanamke asishiriki katika harakati za kijamii au kutokuwa kadhi au kiongozi basi lazima awe na Ushahidi.” Sheikh Khamis amesema maana yake ni kwamba hakuna pingamizi ya wanamke kuwa kiongozi au kuwepo kwa masuala ya kusema hili halifai.

Dkt Mzuri Issa ni Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar – TAMWA-Z amekuwa akizungumzia suala la usawa na ushirikishwaji wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi anasema .”Kikatiba wanawake wanahaki ya kuwa kwenye sehemu za maamuzi, ni ukweli usioficha kuwa wanawake wanakuwa huru kuzungumza na wanawake wenzao kuliko wanaume hususan kwenye matatizo kama hayo ambayo yanayowakumba zaidi wanawake “Dkt Mzuri anaendelea kusema kuwa kukosekana kwa wanawake kwenye sehemu za maamuzi inaweza kuwa wanawake hawaridhiki na maamuzi yanayotolewa “Ikiwa wanawake wanakosekana kwenye vyombo vya maamuzi ambavyo vinawajibika kwenye masuala haki basi hapo hakuna utekelezaji wa haki,wala usawa na inawavunja moyo sawa wanawake waliosomo kwenye kada hizo wakikosa nafasi za kushirikishwa au kupatiwa nafasi naweza kusema hawatendewi haki” Amemalizia Dkt Mzuri Issa.

Amina Salum Khalfan ni Mwanarakati wa Kiislam anapingana na mawazo ya viongozi wa dini wasioamini nafasi ya mwanamke kwenye masuala ya kijamii na upatikanaji wa haki. “Nikiletewa kesi nawaambia nendani ofisi ya Kadhi au ya Mufti wanawake wanakataa kwa sasa huwezi kuzungumza faragha zako za ndani zinamhusu mwanaume mbele ya wananaume wenzao ni aibu na sio jambo linakubalika kidini “Anaendelea kusema “Kuna madhara makubwa ikiwa wanawake hawatapata nafasi kwenye sehemu hizo maana dini haijasema hivyo, wanaona uzito kwenye suala hili maana waliowengi wameshikilia dini na kukosa maarifa ya hio dini lakini zaidi ni mitazamo yao” Amemalizia kusema Amina.

Mwaka 2019 kupitia Baraza la Wakilishi kulizuka mjadala mkubwa juu ya suala la wanawake kupatiwa nafasi kwenye sehemu za maamuzi huku baadhi ya wawakilishi wakipinga suala hilo kwa kunasabisha dini kukataza baadhi ya masuala ya wanawake kuwa hawafai kuwa kwenye baraza la Maulama .Novemba 27, 2019 kupitia kikao cha kwanza,Mkutano wa 16 wakati wa kuwasilisha Mswada wa Marekebisho ya Kuanzishwa Afisi ya Mufti Nam.9 ya Mwaka 2001 ambao kupitia kikao hicho wajumbe wa Baraza la Wakilishi walijadili kuhusu nafasi ya kuwepo wa maulamaa wanawake.

Akichangia muswada huo Rashid Makame Shamsi ambaye alikuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni alihoji juu ya kuwepo kwa wajumbe 16 wanaume katika baraza la Maulama “Sasa Wajumbe waliotajwa katika Baraza hilo ukipiga mahesabu ni wajumbe 16, sasa ndani ya Wajumbe 16 ni Masheikh, Shekhe mmoja mmoja kutoka kila wilaya na wilaya tuna 10. Sasa ukitizama sitarajii kwamba ndani ya hao Masheikh watakuwemo Masheikh wanawake sitarajii. Kwa sababu ulamaa ni mtu mwenye elimu ya juu katika uwanja wa dini kwa mujibu wa kamusi zote za kiswahili na watu wenye upeo wa dini ya kiislamu wanawake hivi sasa wako wengi sana na kazi kubwa sio kutoa fatwa ni kumshauri Mufti wa Zanzibar.Mimi sifikirii kabisa na nimefanya utafiti kwa Masheikh maulamaa na wasomi wa dini ya kiislam suala hili halina madhara kuwaingiza wanazuoni wanawake katika Baraza la Maulamaa la Zanzibar” Alimalizia Rashid Makame Shamsi – Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni- Zanzibar.

Kupitia Hansad za Baraza la Wakilishi Zanzibar aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalimu akijibu hoja na wajumbe waliochgia mjadala huo aliunga mkono hoja ya kufanyika kwa marekebisho ya baadhi ya vifungu hivyo na wanawake wapate nafasi ya kuingia kwenye Baraza ma Ulamaa kupitia Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar “hili la uanzishwaji wa Baraza la Ulamaa, sisi binafsi ushauri huu ulitolewa awali kuona uwezekano pengine na akina mama waweze kuwemo katika Baraza hili.Lakini vile vile, tuangalie uwezekano kwamba kina mama wanaweza kwamba hapa wasiorodheshwe kwamba wawepo katika hii sheria na mimi naungana nao moja kwa moja kwamba ziwepo pengine nafasi mbili za kina mama za wanawake katika Baraza hili.” Alimalizia kuchangia hoja hio.

Jamila Mahmoud ni Mkurugenzi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Zanzibar – ZAFELA amesema suala la kuwepo kwa msisitizo wa kuchaguliwa na kupatiwa nafasi kwa Maulama wanawake halipo kisheria hivyo hio ni miongoni kwa sababu kubwa ya wanaotoa nafasi cha kuchagu kuona hili jambo sio lazima na halina umuhimu “ Kwa mfano Sheria ya Mahakama ya Kadhi yam waka 2003 Kifungu cha 10(4) “Sheri ya Ofisi ya Mufti wa Zanzibar yam waka 2021 kwenye kipengele cha ufafanuzi imefafanua Ulamaa kuwa ni “ Mwanachuoni wa Kiislamu mwenye elimu ya kutosha ya fani mbalimbali ya dini ya kiislam na lugha ya kiarab”. Hapana hakuna sehemu iiyowekwa jinsia maana wanawake na wanaume wenye uwezo wa kielimu wapewe nafasi.

Jamila ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwenye suala la wanawake Maulama kutokuwepo kwenye ngazi za maamuzi ni kwa sababu wanaopata nafasi za kuwateuwa hao maulama bado wanaamini kwenye mifumo dume”. Amemalizia Jamila.

Ofisi ya Mufti Mkuu kutokuwateua wanawake kwenye baraza la Maulamana Sheikh Khalid Ali Mfaume ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar amesema wao hawana jukumu la kuwapatia wanawake nafasi ila Serikali ndio inajukumu hilo na pia serikali inazingatia vigezo maalum vya kupewa ajira. “Wanawake wanamchango wao kwenye jamii ila bado suala la wanawake kuwa kwenye baraza la ulama ani suala ambalo linahitajika kufanyiwa kazi” Alimalizia Sheikh Khalid.


*MWENYEKITI Lee Man-hee -Jukumu langu ni kushuhudia matukio ya Ufunuo kama nilivyoyasikia na kuyaona."

*Ushuhuda juu ya ukweli uliotimizwa wa Ufunuo' ulielezea kimantiki na kwa utaratibu.

MWENYEKITI wa kanisa la Shincheonji, Lee Man-hee amesema ikiwa mtu anatamani mbingu na uzima wa milele, ni lazima waende hadi mwisho wa dunia ikiwa ni lazima ili kujua kama ni ukweli unaotimizwa kulingana na Biblia.

Hayo amesema Wakati wa Semina ya bibilia iliyofanyika Barani Asia katika nchi ya Uphilipino Aprili 20, 2024. mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwajulisha wakristo wote kuhusu ukweli uliotimizwa kwenye kitabu cha Ufunuo.

Mwenyekiti Lee alisisitiza, "Imani sio kutafuta pesa," na "Sio wakati wa kuwa na imani na mawazo ya zamani. Mtu lazima athibitishe. Baada ya kuthibitisha, lazima aamue kuamini au la."

"Ni kazi ya mtu huyu kufikisha kile kilichoonekana na kusikika kutoka kwa matukio ya Ufunuo sura ya 1 hadi 22. Nilichokiona na kusikia, kile nilichogusa na kile kilichopo katika hali halisi, ndicho nilichokuja hapa kushiriki nanyi. Sasa sio wakati wa kusema chochote na kukubaliana tu na 'Amina'. Lazima uelewe nyakati za ukweli. Ni wakati ambao ahadi zimetimizwa."

Katika ukumbi wa mihadhara ya ndani huko Ufilipino, makofi yalijaza nafasi, ambayo ilionekana kukaa maelfu kwa mtazamo wa kwanza. Sauti yenye nguvu na hotuba ya ujasiri inayotokana na kimo kidogo, ambayo ilionekana kuwa haiwezekani kwa mtu zaidi ya miaka tisini, ilifanya maneno rahisi hata mtoto anaweza kuelewa. Katika muda mfupi, hali ilizidi kuwa kali. Mtu ambaye alifanya hivyo kutokea hakuwa mwingine isipokuwa Shincheonji Kanisa la Yesu, Hekalu la Hema ya Ushuhuda, Mwenyekiti Lee Man-hee.

Siku hiyo, Mwenyekiti Lee alizindua Semina za Biblia za Shincheonji za 2024 za Bara la Asia (I)' kwa kutembelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ufilipino. Mfululizo wa hotuba utaendelea mwaka mzima huko Ulaya, Afrika, Amerika, Oceania, na kuhitimisha tena Asia (II). Kanisa la Shincheonji la Yesu liliandaa Semina hiyo ya Neno kutokana na majibu mengi na maombi ya dhati kutoka kwa wachungaji na waumini wengi ulimwenguni kote kufuatia 'Semina ya Neno la Ufunuo Shincheonji '.

Akiwa na ukumbi wa mihadhara ambao una viti 4,000 vilivyojaa watu, Mwenyekiti Lee alichukua hatua na kwanza akajitambulisha na kile kilichomfanya aamini. Ilitoa hisia sawa na jinsi waandishi wa kibiblia walivyoanza kuelezea ukoo wao na nyakati kabla ya maudhui kuu

Mwenyekiti Lee alisema kwa nguvu, "Sasa si wakati wa kusema chochote na kukubaliana tu na 'Amina,'" na "Lazima uelewe nyakati ya ukweli. Ni zama ambazo ahadi zimetimizwa." Alisisitiza, "Ufunuo unatia ndani mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumi, na pia nyota saba. Ni juu ya kuelewa kile ambacho kuonekana kwa kweli kunawakilisha," na akasisitiza kwamba "wakati Mungu anaandika kuibuka kwa watu kama hao, ni ili leo utimizo utimie. kuona, kusikia, na kuamini."

Akirejelea Ufunuo 22:18-19, Mwenyekiti Lee alisisitiza mara kwa mara kwamba mtu hawezi kuingia mbinguni ikiwa wataongeza au kuondoa kutoka kwa Kitabu cha Ufunuo. Kwa kufanya hivyo, aliamsha hisia ya uharaka katika imani kwa kusema, "Mtu lazima ajue kila kitu bila kupunguza. Ni vigumu kutosha kufanya mazoezi hata wakati wa kujua kila kitu; bila ujuzi, mtu angeweza kupoteza matumaini."

Pia alikazia kwa mara nyingine tena kwamba ni lazima mtu afahamu kikamili Ufunuo na kutiwa muhuri kana kwamba anapigwa muhuri. Mwenyekiti Lee aliuliza, "Kwa nini unafikiri imeandikwa katika Ufunuo 22:18-19 kwamba mtu hataingia katika ufalme wa mbinguni na atalaaniwa ikiwa ataongeza au kupunguza kutoka humo?" Akajibu, "Ni kwa sababu maneno haya yanatimia kana kwamba yanapigwa muhuri."

Mwenyekiti Lee alisisitiza umuhimu wa kuandika maneno katika moyo wa mtu, kuwa 'Biblia inayotembea' na 'neno lililo hai.' Alitaja kwamba wale wanaofanya hivyo wanakuwa wale waliotiwa muhuri wanaotajwa katika Ufunuo 7, ambao wameokolewa. Mwenyekiti Lee alitangaza, "Hakuna wokovu unaotajwa isipokuwa wale waliotiwa muhuri 144,000 na kundi kubwa la watu waliovaa mavazi meupe; mtu ye yote ambaye hajatiwa muhuri anakuwa kama udongo, asiye na uhusiano wowote nalo. Ni wale tu waliotiwa muhuri wanaweza kuingia ufalme wa mbinguni." Pia alisema kwa uthabiti, "Wale ambao wametiwa muhuri wanaweza kuishi mbinguni, kuwa na uzima wa milele, na kuwa sehemu ya familia ya Mungu, lakini wale ambao hawana basi hawana uhusiano na Mungu."

Kwa wenyeji, Mwenyekiti Lee mara kwa mara aliwasilisha salamu kama vile "Nina uhusiano wa kina na Ufilipino," "Ufilipino ilikuwa mahali pa kwanza nilipokuja kutoa ushahidi baada ya kupokea neno," na "Ninaipenda sana Ufilipino.

Kwa kweli, Ufilipino imedumisha uhusiano na Mwenyekiti Lee kwa zaidi ya muongo mmoja. Mbali na shughuli zake za kidini, akiwa mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la HWPL (Heavenly Culture, World Peace, Restoration of Light), alitembelea Ufilipino na kupatanisha makubaliano ya kwanza ya amani ya kiraia huko Mindanao, ambayo yamekuwa katika migogoro kwa muda mrefu. miaka 40. Kufuatia hili, amani ilianzishwa katika kanda, na habari hii ilipata tahadhari ya kimataifa.



ZANZIBAR
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma umeshiriki kwenye Mkutano Mkuu wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Zanzibar na kupata fursa ya kuelimisha kupitia maonesho na uwasilishaji wa mada kwa wajumbe wa mkutano Mkuu.

Mkutano huo muhimu hujumuisha Wenyeviti wa Mikoa na Halmashauri zote nchini, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa zote nchini, Mameya, na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya ALAT.

Meneja wa Ofisi ya Zanzibar wa PSSSF, Bi. Amina Kassim aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuhusu maboresho ya kidijitali yaliyofanywa na PSSSF ili kuboresha huduma kwa wateja ikiwemo kuhusu mfumo mpya wa kupokea madai ya mafao mtandaoni na usajili wa wanachama mtandaoni.

Aidha aliwaomba waendelee kutoa ushirkiano ili kutatua changamoto za kiutendaji kwa wakati.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa na kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi yanRais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed.

Mkutano Mkuu umehudhuriwa na wajumbe na taasisi wadhamini takribani 450.






WAANDISHI wa habari wametakiwa kupaza sauti zao kuwatetea wananchi kupitia vyombo vya habari kwa maslahi ya kukuza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ambao utasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa taifa.

Uhuru huo unaweza kupatikana endapo kutakuwa na sheria rafiki za habari sambamba na waandishi wenyewe kufanya kazi kwa kufuata maadili ya tasnia yao na kuendeleza jukumu la huleta maendeleo kutokana na kuwa kiungo cha kupaza sauti kwa wasio na sauti .

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA-ZNZ) Dkt Mzuri Issa Ali wakati wa mafunzo ya siku moja ya kupitia Mikataba ya kikanda na ya Kimataifa na kujadili mapungufu ya sheria zinazokwamisha uhuru wa habari Zanzibar.

Ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo yaliyowakutanisha watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo , Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Tume ya Utangazaji na waandishi wa habari ni kukumbushana umuhimu wa kuangalia ni kwa kiasi gani kama nchi imeweza kuzingatia mikataba hiyo ili kupata sheria na sera bora zitakazo simamia masuala ya haki ya kupata habari na kutoa maoni na kukuza demokrasia nchini .

Aidha amebainisha kuwa pamoja na kuridhia Mikataba ya bado sauti za wananchi hazipewi kipau mbele kusikika katika vyombo vya habari ukilinganisha na sauti za viongozi jambo ambalo linawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni.

Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights (UDHR), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (The International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR) na Mkataba wa Haki za Binadamu na Haki za Watu wa Umoja wa Afrika (African Charter on Human and Peoples Rights - ACHPR)

“Nchi nyingi za Afrika zimeweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa kuvitumia vyema vyombo vya habari kwa uhuru na kupelekea kuinua uchumi wa nchi ambapo ni pamoja na Ghana, Afrika ya kusini na Mozambique.

Mapema akiwasilisha mada kuhusiana na “Mapungufu ya Sheria za habari” Bibi Hawra Shamte ambae ni mwandishi wa habari mkongwe amesema ingawa kuna sheria zinazosimamia sekta ya habari bado zinaonekana kiuhalisia hazifanyi kazi ipasavyo kwa kulinda usalama wa waandishi wa habari na wananchi hivyo zinahitaji kufanyiwa marekebisho.

“Baadhi ya sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu No. 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya mwaka 1997 na Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar No. 7 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No 1 ya 2010”, alieleza muwasilishaji huyo.

Wakichangia katika mafunzo hayo, miongoni mwa waandishi wahabari wamesema wamaekuwa wakikutana na vikwazo mbalimbali katika kufanikisha majukumu yao, hali inayosababisha kukosa uhuru na kutowajibika ipasavyo.

Mafunzo hayo yametolewa na TAMWA-ZNZ kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo,Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Tume ya Utangazaji na waandishi wa habari yenye lengo la kuonesha umuhimu wa kuzingatia mikataba ya kikanda na ya kimataifa ili kuwa na sheria na sera bora zitakazo simamia masuala ya haki ya kupata habari na kutoa maoni kwa uhuru.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Parimatch Levis Paul akizungumza machache mara baada ya Kuzinduliwa kwa Msimu wa tatu wa Shindano la Bingwa ambapo msimu huo Kampuni hiyo ikiwa wadhamini wakuu wa shindano.
 Meneja programu wa shindano la Bingwa Ombeni Phiri akieleza namna Shindano hilo litakavyoshirikisha Mikoa mitano ambayo ni Arusha,Mbeya,Mwanza,Dodoma pamoja na Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Aprili 24,2024  Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam  wakati wa Uzinduzi wa Msimu wa tatu wa Shindano la Bingwa ambapo amewataka wateja wa Kisimbuzi cha Startimes kulipia kifurushi ili kuendelea kuona shindano hilo kupitia Tv3

SHINDANO la Mtindo wa Maisha (Life style) Kwa Vijana wenye ushawishi Mitandaoni ( BINGWA ) Msimu wa tatu umezundiliwa rasmi Vijana Mikoani wapewa nafasi .

Akizungumza na Wanahabari Leo Aprili 24,024 Ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua Shindano hilo kwa Msimu wa tatu Meneja wa Shindano hilo Ombeni Phiri amesema Shindano hilo limewapa fursa Vijana wengi mitandaoni kubadilisha maisha kutokana na fursa mbalimbali ambazo wamekuwa wakizipata na hivyo kulazimika Shindano hilo kuendelea kuwepo ambapo msimu huo wa tatu umekuwa wa kitofauti zaidi.

"Misimu miwili imekuwa yenye Mafanikio makubwa zaidi na Vijana wengi wa mitandao kuonesha Maisha yao halisi wanapokuwa kwenye mjengo huo hivyo kwa Msimu huu watatu Umepewa nguvu na Kampuni ya Kubashiri ya Parimatch ili kumsukuma Mshindi huyo kufanya vitu vikubwa zaidi Pape Shindano linapomalizika

Msimu Mpya wa tatu wa show ya Bingwa itatembelea Mikoa mitano kwa ajili ya kutafuta Vijana wengine ambapo maoni mengi yamekuwa yakiwafikia Vijana wakihitaji kushiriki Shindano hilo.

"Msimu wa tatu umefanya Maboresho mbalimbali ikiwemo ongezeko la Mikoa mitano ya washiriki ikiwemo Arusha, Dodoma,Mwanza, Mbeya pamoja na kitovu chenyewe Dar es Salaam.

Pia ameeleza kuwa usahili kila Mkoa utachukua washiriki 10 kila Mkoa na kufatia mchujo katika App ya Startimes (Startimes On) ambapo washiriki 08 watatoka Dar hivyo kukamilisha Jumla ya watakaoingia ndani ya nyumba washiriki 24 huku zawadi ya Mshindi kugharimu zaidi ya Milioni 35 za Kitanzania.

Kwa Upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema Msimu wa tatu utaendelea kuwapa fursa vijana zaidi na Atakaeibuka Mshindi Kampuni ya Startimes itaweza kumpa Ubalozi.

Aidha amewapongeza Kampuni ya Parimatch kuona haja ya kuwapa Moyo Vijana hao wenye ushawishi Mitandaoni kukuza vipaji vyao.

Pia amewataka wateja kulipia vifurushi cha Uhuru elfu 23000 ili kuweza kuona shindano hilo kupitia Tv3 ndani ya King'amuzi cha Startimes.

Nae Meneja Masoko wa Parimatch Levis Paul ameeleza sababu ya Kampuni hiyo kuishika mkono Shindano hilo la " Bingwa".

"Sababu ya Parimatch kuungana na Msimu wa tatu wa Shindano la bingwa ni kutokana na shindano hilo Kuhusisha Vijana na Kauli mbiu ikibeba Jumba la Washindi ambapo Kampuni yetu inalenga zaidi kutafuta Washindi walipo kwa kupitia ubashiri."

Paul ameeleza wao kama Parimatch wanatambua kuwa Washiriki wanahitaji kukaa siku 70 ambapo kila kitu kinahitaji uwezeshwaji kuanzia Malazi na vitu mbalimbali hivyo Tv3 na Startimes peke wanahitaji nguvu ya ziada ya kuendesha Shindano hilo hivyo sisi tumeona tuongeze nguvu hiyo kwa msimu huu wa tatu."

Pia amefafanua zaidi kuwa Wana amini kuwa chapa ya Kampuni hiyo ipo sehemu na sahihi hivyo kudhamini shindano hilo itaongeza na kujiweka kwenye nafasi nyingine nzuri zaidi ya kujitangaza kama Kampuni.

Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kuwa ina lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tarafa hiyo kwa kuwaelimisha na kuwahamisha wananchi waliojiandikisha kuhama kwa hiyari kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga na maeneo mengine nchini.

Akizungumza na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwa nyakati tofauti katika zoezi la uelimishaji, uhamaishaji na uandikishaji kaimu meneja wa Uhusiano kwa Umma wa mamlaka hiyo Hamis Dambaya amesema zoezi la kuwaelimisha wananchi hao litaendelea ili kuhakikisha kila mkazi wa tarafa ya Ngorongoro anahama kwa hiyari. 

Amewaeleza wananchi hao kwamba serikali haina nia mbaya kwa kuwashawishi kuhama kutoka ndani ya hifadhi kwani inatambua kuwa iwapo wananchi hao watakubali kuhama wataweza kuboresha maisha yao katika maeneo mbalimbali watakayoamua kuelekea sambamba na kulinda usalama wao kutokana na uwepo wa matukio ya wanyama wakali ndani ya hifadhi. 

“Mnaishi katika mazingira magumu hasa kutokana na kukosa uhuru wa kuingia na kutoka ndani ya hifadhi, kuhofia Wanyama wakali ambao wamekuwa hatari kwa mifugo na baadhi ya wananchi, serikali imefanya uamuzi sahihi wa kuwahamasisha ili kuwa na Maisha bora na huru nje ya hifadhi,”alisema bwana Dambaya.

Bwana Dambaya amesisitiza kuwa serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mwananchi anayekubali kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi anapata stahiki zake zote za kisheria ikiwemo kitita cha shilingi milioni kumi wanaohamia msomera na shilingi Milioni kumi na tano wanaohamia maeneo mengine ambapo fedha hizi zinatolewa kama motisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Amewataka wananchi hao kuachana na propaganda za baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wasiowatakia mema kwa kuwashawishi kuendelea kubaki ndani ya hifadhi huku wao na familia zao wakiishi katika miji mbalimbali nchini na kufanya shughuli zao katika mazingira magumu.

“Msihadaike na watu wenye nia ovu wanaowashawishi mbaki ndani ya hifadhi, hameni kwa hiyari kuelekea katika Kijiji cha Msomera na maeneo mengine ambayo huduma za kijamii zimeboreshwa kwa mustakabali wenu na vizazi vyenu”,alisema bwana Dambaya.

Katika ziara hiyo ya tarafa ya Ngorongoro timu ya uhamasishaji imeweza kutembelea kaya mbalimbali katika Kijiji cha Naiyobi, Kapenjiro na endulen ambapo wananchi kadhaa walielimishwa na kukubali kuhama kwa hiyari na kuamua kujiandikisha.





Na Mathias Canal

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 66 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika nchini.

Fedha hizo tayari zimegawanywa kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote iliyoathirika kwa ajili ya kufanya kazi kwa haraka usiku na mchana ili kurekebisha kadhia zilizozikumbumba barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Akizungumza jana Jijini Arusha mara baada ya kukagua Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha bypass) iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mha. Mohamed Besta amesema kuwa kutokana na udharula huo tayari Rais Samia ametoa fedha za matengenezo ya miundiombinu hiyo ambazo zimeshapelekwa katika Mikoa yote Nchini.

Mhandisi Besta amesema kuwa tayari kazi inaendelea katika maeneo yote nchini na fedha hizo zinaratibiwa na vitengo maalumu vya dharula vilivyopo TANROADS pamoja na ofisi za mikoa.

Ameongeza kuwa kutokana na tathimini iliyofanyika mpaka sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 250 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Barabara kuu za Mikoa yote Nchini ambazo zimeharibika vibaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo kama Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini mwa Nchi mvua zimeendelea kunyesha tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na sasa unaelekea mwezi wa saba na mvua bado zinaendelea kunyesha.

“Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ametupatia shilingi bilioni 66 ambazo tumezisambaza katika Mikoa yote ambapo mameneja wote wa Mikoa wamepewa kutokana na hali ya dharura ya Mkoa husika’’ ameeleza

Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha Mhandisi Regnald Massawe amesema Mkoa huo umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kazi hizo za dharura na matengenezo ya kurejesha miundombinu hiyo yanaendelea kufanyika kwa kasi.







MKUTANO wa 5 wa Harvard Kennedy School China umefanyika katika Shule ya Harvard Kennedy Usiku wa tarehe 21, Pang Xinxing, Mwenyekiti wa Startimes Group, alialikwa kuhudhuria mtandaoni.

Aidha Lengo Mkutano huo ni kujenga daraja la mawasiliano kati ya China na ulimwengu, kutoa jukwaa rafiki na wazi kwa majadiliano kati ya academia ya kimataifa, serikali, biashara, na viongozi wa jamii.

Kauli mbiu ya mkutano huu ilikuwa "Uaminifu na Ushirikiano," ukiwa na vikao tisa vinavyojadili mada kama "Mahusiano ya Marekani na China," "Uchumi wa Dunia na Uchumi wa China," "Utawala wa Dunia wa Akili Bandia," "China na Kusini Mashariki mwa Asia," "China na Mashariki ya Kati," "China na Afrika," "China na Amerika Kusini," miongoni mwa mengine.

Hafla hiyo ilialika Xie Feng, Balozi wa China nchini Marekani, Graham Allison, mwanzilishi wa Shule ya Harvard Kennedy Graham Allison, Dean Xue Lan wa Chuo Kikuu cha Tsinghua cha Schwarzman, pamoja na wawakilishi kutoka kwa sekta za kisiasa, biashara, na kitaaluma za nchi zote mbili, zaidi ya wanafunzi na wanachama 300 wa fakulteti wa Harvard, na zaidi ya wanafunzi 300 wa Kichina wanaosoma nchini Marekani.

Kupitia mawasiliano na ushirikiano, mkutano ulilenga kupata njia za pamoja za maendeleo.

Kama mwanzilishi wa kampuni inayoongoza ya televisheni ya kidigitali barani Afrika, Pang Xinxing, Mwenyekiti wa Startimes Group, alitoa hotuba mtandaoni katika kikao cha "China na Afrika: Matarajio ya Baadaye," akishiriki safari ya kuanzishwa, kukua, na maendeleo ya biashara ya Afrika ya Startimes Group na washiriki.

Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa kikihusika sana katika uga wa utangazaji, televisheni, na vyombo vya habari vipya.


Mwenyekiti Pang Xinxing alitambulisha: "Nchini China, StarTimes imepitia mchakato mzima wa maendeleo ya televisheni ya waya ya Kichina, kutoka kutokuwepo hadi kuwepo, kutoka analogia hadi kidijitali, ikawa msanidi wa mfumo na mtoa teknolojia mwenye athari kubwa katika tasnia ya redio na televisheni ya Kichina."

Barani Afrika, kuanzia kupata leseni ya kwanza ya uendeshaji wa televisheni ya kidigitali nchini Rwanda mwaka 2007, baada ya miaka karibu ishirini ya uendeshaji na maendeleo, "StarTimes imesimamisha jukwaa la usambazaji wa mtandao linalofunika nchi 45 na watu bilioni 1.2 katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Imekuwa kampuni pekee inayotoa huduma za video ndefu za kulipia katika mikoa inayozungumza Kiingereza, Kifaransa, na Kireno barani Afrika kwa wakati mmoja.

Imesimamisha mfumo wa uzalishaji wa yaliyomo kupitia ujumuishaji wa programu, tafsiri ya programu, na uzalishaji wa programu, sasa ikipeperusha seti 830 za vituo vya televisheni vya Kiafrika vya kimsingi, vituo vilivyoendeshwa na StarTimes, na vituo vya kimataifa kwenye jukwaa katika lugha zaidi ya kumi kwa matangazo ya 24 masaa kwa siku.


Imesimamisha mfumo kamili wa masoko na mfumo wa huduma baada ya mauzo, ikiwa ni pamoja na maduka zaidi ya 200 na maduka ya urahisi zaidi ya 30,000, na imeunda wafanyikazi wa 4,000."
Aliyaeleza: "StarTimes imekuwa ikifanya uwekezaji endelevu katika tasnia ya habari ya Afrika na kutoa mchango wake katika digitalization na habari za jamii ya Kiafrika," ikiwa ni pamoja na kuvunja monopolies za tasnia, kukuza upanuzi wa televisheni ya kidigitali barani Afrika, kupunguza kwa kiasi kikubwa vikwazo vya uwekezaji na teknolojia kwa vyombo vya habari vya televisheni vya eneo hilo, kukuza utajiri na maendeleo ya vyombo vya habari vya Kiafrika vya eneo hilo, kuandaa mashindano ya kudubu lugha za Kiafrika ili kuchagua na kutoa mafunzo kwa vipaji vya kudubu vya eneo hilo, kuanzisha vituo vya kudubu katika makao makuu ya StarTimes na mahali pengine barani Afrika kukuza urithi na maendeleo ya utamaduni wa Kiafrika wa eneo hilo, na zaidi.


Leo, StarTimes imekuwa chapa inayojulikana sana barani Afrika Katika ushirikiano unaongezeka kati ya China na Afrika leo, uendeshaji wa StarTimes barani Afrika unaingia kwenye kipindi cha mavuno. Mwenyekiti Pang Xinxing alibainisha, "Kwa kina cha ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya China na Afrika na kuongezeka kwa usaidizi kwa miundombinu ya nishati barani Afrika na mashirika kama Benki ya Dunia, umeme barani Afrika unazidi kuwa wa kawaida.

Kadiri inavyoendelea, muongo ujao bila shaka utakuwa muongo wa upanuzi wa vituo vya kidigitali (vya akili) vya nyumbani barani Afrika. Tuna imani kamili katika maendeleo ya uchumi wa Kiafrika!"
Mwenyekiti Pang xing xing wa  StarTimes Group akitoa hotuba kwenye mkutano) Mkutano wa Harvard Kennedy School China, ulioanzishwa na Chama Kikuu cha Harvard Kennedy Greater China, unazingatia maendeleo ya uchumi, siasa, na utamaduni wa China na nchi za nje
(Washiriki wakisikiliza hotuba na kujadiliana na Mwenyekiti Pang)
Startimes Group ilianzishwa mwaka 1988 na kina historia ya miaka 35.

Na Mwandishi wetu

Matumizi ya Mfumo wa kuwezesha uratibu wa shughuli za uandaaji wa vikao mbalimbali vya bodi na menejimenti katika Halmashauri na Taasisi za Umma. (e-Board), umetajwa kurahisisha uendeshaji wa vikao na kupunguza gharama za maandalizi katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza.

Akizungumza kuhusu mfumo huo ofisini kwake jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi. Ummy Mohammed Wayayu, amesema kuwa kabla ya halmashauri hiyo kuanza kutumia mfumo wa e-Board mwaka 2023, fedha nyingi zilikuwa zinatengwa katika ununuzi wa shajara,wino na vifaa vingine kwa ajili ya vikao vya madiwani na menejimenti.

“Kwa mwaka tulikuwa tunatumia takribani shilingi milioni 200 hadi 300 katika maandalizi ya uendeshaji wa vikao, lakini kwa sasa gharama hizo hatuna tena kwakuwa tunatumia mfumo huu wa e-Board, ambao umetusaidie kupeleka fedha hizo katika mambo mengine ya muhimu katika halmashauri,” alisema Bi.Ummy.

Aliongeza kuwa, mfumo wa e-Board umesaidia kupunguza gharama za kudurufu taarifa mbalimbali na badala yake zinapakiwa kwenye mfumo na madiwani wanapakuwa na kuendelea kuzifanyia kazi.

Licha ya mfumo huo kusaidia katika kupunga gharama, Mkurugenzi huyo amesema kwamba mfumo wa e-Board umesaidia katika upigaji wa kura za siri katika uchaguzi wa Wenyeviti wa Kamati pamoja na uchaguzi wa Mstahiki Meya.

“Hapo awali usiri katika chaguzi hizo ulikuwa mdogo sana, lakini kwa sasa tunatumia mfumo hivyo kura zinakuwa za siri na kila mtu ndani ya nafsi anajua amemchagua nani,” alifafanua.

Aidha, Bi Ummy aliongeza kuwa mfumo wa e-Board unawasaidia madiwani kushiriki katika kila kikao hata wanapokuwa nje ya halmashauri hiyo kwa kutumia vishkwambi ambavyo vimewezeshwa matumizi ya mfumo huo na kugawiwa kwa kila diwani.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Renatus Mulunga, alisema kuwa mfumo wa e-Board umewasaidia madiwani kuendesha vikao vyao kwa ufanisi ili kuboresha huduma za wananchi wa Ilemela.

“Nina miaka 25 kwenye udiwani, huko nyuma ilikuwa lazima ujaze gari mafuta kwa ajili ya kusambaza makarabrasha, lakini kupitia mfumo wa e-Board kila diwani anapata taarifa na makabrasha yake popote alipo kupitia mfumo na kuanza kuyafanyia kazi,” alisema Bw. Mulunga.

Mhe.Mulunga alitoa rai kwa halmashauri nyingine ambazo bado hazijaanza kutumia mfumo wa e-Board, kufanya ziara halmashauri ya Manispaa ya ilemela ili zikajifunze au kuwasiliana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ili zipate uelewa kuhusu mfumo huo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Halmashauri ya Ilemela Bw.Isaack Tanguye, alisema kwamba halmashauri hiyo ilianza kutumia mfumo wa e-Board baada ya kupata malalamiko kuhusu gharama kubwa za uandaaji wa vikao.

Alisema kwamba baada ya malalamiko hayo kuwa mengi, kitengo chake kiliamua kuwasiliana na e-GA kuomba mfumo wa e-Board, na baadaye walianza kuwajengea uwezo Madiwani pamoja na Menejimenti ya halmashauri hiyo ili kuanza kufanya vikao vyao kidijiti.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ndiyo halmashauri ya kwanza kuanza kutumia mfumo huu wa e-board kati ya halmashauri 184 nchini, mfumo huu umesanifiwa na kutengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).


Top News